Tuesday, 3 May 2016

KILIMANJARO:Mkuu wa wilaya ya moshi awataka wajasiriamali kutengeneza bidhaa bora...............

MKUU wa Wilaya ya Moshi, Norvatus Makunga, amewataka wajasiriamali wadogo mkoani Kilimanjaro, kutengeneza bidhaa zenye ubora inayolingana na thamani halisi, kwa kupunguza uagizwaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Makunga aliyasema hayo jana mjini Moshi, wakati akifunga mafunzo ya wiki mbili ya wajasiriamali wadogo, wa fani mbalimbali kutoka wilaya za Moshi, Mwanga na Rombo, ambapo yaliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO).
Alisema tatizo kubwa la baadhi ya wajasiriamali wadogo hapa nchini, wamekuwa wakizalisha bidhaa nzuri lakini zimekuwa zikikosa ubora unaohitajika kwenye mahitaji ya soko, hali inayowafanya wafanyabiashara kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi.
Makunga alisema ubora wa bidhaa ndio nguzo muhimu ya kuweza kukuza soko la ndani na nje ya nchi, ambapo aliwataka wajasiriamali hao kujifunza na kujiimarisha zaidi, ili waweze kuwa washindani wazuri katika soko la Afrika masariki Mmoja wa wajasiriamali katika mafunzo hayo, Gloria Mosha, alisema changamoto inayowakabili wajasiriamali wadogo ni wafanyabiashara wakubwa kuagiza bidhaa nje ya nchi, ambapo bidhaa hizo zimekuwa zikitengenezwa hapa nchini, hali inayosababisha wajasiriamali kukosa soko la ndani.
Mosha alisema licha ya ubora wa baadhi ya bidhaa za ndani kutokidhi mahitaji ya soko la dunia, changamoto kubwa wanayokumbana nayo pia ni ukosefu wa nishati ya uhakika, hali inayosababisha ufanyaji kazi kuzorota kutokana na umeme kukatika mara kwa mara.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO), Arthur Ndedya, aliwataka washiriki hao kutumia mafunzo hayo, kwa lengo la kuboresha bidhaa zao zikidhi viwango vya ushindana wa masoko la dunia

No comments:

Post a Comment