Saturday, 28 May 2016

BURUDANI:SHINDANO LA MAISHA PLUS MSIMU WA 5 LAZINDULIWA RASMI, KUONYESHWA MOJA KWA MOJA NA AZAM TV

MAS1Mkurugenzi wa Azam Media  Tido Mhando (Kushoto) akizungumza  wakati wa uzinduzi wa Maisha Plus East Africa Mkurugenzi wa  Maisha Plus East Africa msimu wa 5 ambapo shindano linatarajiwa kuanza hivi karibuni itakapotangazwa ratiba ya kutafuta washiriki wa shindano hili mikoani na nchi zingine za Afrika Mashariki,  kulia ni mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw. Masoud Kipanya, Masoud Kipanya ni  miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus na mtangazaji wa kipindi hicho ambacho  huandaliwa na kampuni ya DMB Company Limited na mwaka huu inandaa kwa udhamini mkubwa wa  Azam Media, Hafla ya uzinduzi huo  ilifanyika jana katika studio za Uhai Productions – Azam, Tabata jijini  Dar es salaam.
mas13
Joyce Fisoo Katibu Mtendaji wa  bodi ya filamu Tanzania akizungumza mawili matatu wakati wa uzinduzi huo kama mgeni mwalikwa lakini pia kama mdau muhimu wa shindano hilo.
MAS3Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo
MAS4Mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw. David Seburi akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
MAS7
Baadhi ya waandaji wa shindano la Maisha Plus kulia Francis Bonga na David Sevuri wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana.Jikho Man na Vitalis Maembe wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana.
MAS10Mwandaaji wa shindano hilo Bw. Masoud Kipanya akizungumza na baadhi ya washiriki waliowahi kushiriki katika shindano hilo kulia ni Abdul aliyekuwa mshindi.mas12Aliyewahi kuwa mshindi wa shindano hilo Abdul akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika jana.
MAS11Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakiwa katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment