Saturday, 28 May 2016

KUTOKA MOSHI:WANANCHI WAFURIKA BANDA LA BENKI YA NMB KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI.

Mgeni Rasmi katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji,Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala manispaa ya Moshi,Wencelaus Lindi akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Benki ya NMB katika maeonesho hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya biashara na Kilimo wa Benki ya NMB,Oscar Rwechungura (aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi ,Wencelaus Lindi (aliyekunja mikono) katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yaliyoandaliwa na Mtandao wa kusaidia wakulima wa AgriProFocus.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi,Emanuel Kashusho akikabidhi zawadi ya T-shirt ,Kalamu na Key holder kwa mgeni rasmi ,Wencelaus Lindi mara baada ya kutembelea banda la Benki hiyo na kupata maelezo namna inavyoshirikiana na wakulima katika kukuza mitaji yao.
Mgeni rasmi ,Wencelaus Lindi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wananchi wengine waliofika kutembelea banda la NMB.

BURUDANI:SHINDANO LA MAISHA PLUS MSIMU WA 5 LAZINDULIWA RASMI, KUONYESHWA MOJA KWA MOJA NA AZAM TV

MAS1Mkurugenzi wa Azam Media  Tido Mhando (Kushoto) akizungumza  wakati wa uzinduzi wa Maisha Plus East Africa Mkurugenzi wa  Maisha Plus East Africa msimu wa 5 ambapo shindano linatarajiwa kuanza hivi karibuni itakapotangazwa ratiba ya kutafuta washiriki wa shindano hili mikoani na nchi zingine za Afrika Mashariki,  kulia ni mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw. Masoud Kipanya, Masoud Kipanya ni  miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus na mtangazaji wa kipindi hicho ambacho  huandaliwa na kampuni ya DMB Company Limited na mwaka huu inandaa kwa udhamini mkubwa wa  Azam Media, Hafla ya uzinduzi huo  ilifanyika jana katika studio za Uhai Productions – Azam, Tabata jijini  Dar es salaam.
mas13
Joyce Fisoo Katibu Mtendaji wa  bodi ya filamu Tanzania akizungumza mawili matatu wakati wa uzinduzi huo kama mgeni mwalikwa lakini pia kama mdau muhimu wa shindano hilo.
MAS3Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo
MAS4Mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw. David Seburi akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
MAS7
Baadhi ya waandaji wa shindano la Maisha Plus kulia Francis Bonga na David Sevuri wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana.Jikho Man na Vitalis Maembe wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana.
MAS10Mwandaaji wa shindano hilo Bw. Masoud Kipanya akizungumza na baadhi ya washiriki waliowahi kushiriki katika shindano hilo kulia ni Abdul aliyekuwa mshindi.mas12Aliyewahi kuwa mshindi wa shindano hilo Abdul akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika jana.
MAS11Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakiwa katika hafla hiyo.

KUTOKA MOSHI:MAONYESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YALIYOANDALIWA NA AGRIPROFOCUS YAFANYIKA UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI.

Mgeni Rasmi katika maonesho ya Wakulima na Wagaji ,Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Moshi,Wencelaus Lindi akisoma hotuba ya ufunguzi wa maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa kusaidia Wakulima wa AgriProFocus yanayofanyika katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 
Baadhi ya wananchi wakiwemo wakulima na wafugaji waliohudhuria ufunguzi wa maonesho hayo ya siku Mbili.
Afisa Msaidizi wa  Mtandao wa wadau mbalimbali wanaosaidia wakulima wenye ndoto wa AgriProFocus ,Hildagard Okoth akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Wenceslaus Lindi wakati akitembelea mabanda katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yanayoendelea katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.

HARUSI YA MBUNGE JOSHUA NASSARI NA ANANDE NNKO KANISA LA PENTEKOSTE KALINGA MERU, YAFANA



Msafara wa gari chache majira ya saa 2:30 ulianza safari katika viwanja vya Usa-River ambako gari za maharusi zilikuwa zikipambwa mdogo mdogo zikapanda Kilima zikiwa na maharusi Joshua Nassari na Anande Nnko safari ilikuwa ni kanisa la Kipentekoste la Kilinga,Meru tayari kwa ajili ya Ndoa.…


MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.Kwa Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru...

CloudsFM


Sunday, 8 May 2016

ELIMU:Tuzo za wanafunzi bora Afrika mashariki zaanzishwa "ALL-STARS STUDENTS AWARDS"

Aaron Ally (Dj Aaron Tanzania)Mratibu wa All-stars atudents awards akiongea katika kipindi cha Morning trumpet kuelezea tuzo hizo.
Alhamisi hii alialikwa kwenye kipindi cha morning trumpet cha azam tv kuelezea tuzo hizo zitakazofanyika jijini dar es salaam




Dj wa zamani wa clouds FM,,Aaron,yeye na team yake(Ms Chiku Lweno,Mwl. Danny Mtanga)wameanzisha  tuzo walizoziita All-stars students awards,hizo tuzo zitatolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri o-level na A-level kwa Afrika Mashariki.
Aaron alisema Tuzo hizo zina dhumuni kuwapa hamasa wanafunzi wa shule za Afrika mashariki.Tuzo hizo zitztolewa  kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne na cha sita,pia waalimu husika ambao ni chachu ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye hayo masomo,tuzo hizo zitaangalia wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya kiswahili,hesabu,fizikia,kemia,bailojia na kiingereza.Mchakato huu wa tuzo  utaanza katikati ya mwenzi wa sita pia itaangalia special talents,michezo na shule bora.

Saturday, 7 May 2016

BURUDANI:Mbwa Mzee kawakilisha ndani ya SAFARI NYAMA CHOMA FESTIVAL...............

Nyama Choma Festival Juzi Jumamosi...Chindo & Live Band waliwakilisha Arusha vilivyo...More Fire to Come!!!!Thanks to Carol Ndosi For Counting on me & all ma dogs who were frontline giving me that Energy to Fire Burn.Godbless Y'all.

AFYA:Meya wa jiji a Arusha amekabidhi ambullance..............

Leo Meya Wa Arusha
Mh Kalisti Lazaro amekabidhiwa Rasmi ambulance ya wagonjwa..
Hii nisehemu ya utekelezaji wa ahadi ya mbunge kwa wananchi wake wa Arusha mjini.

MBUNGE WA ARUMERU MASHIRIKI:jOSHUA NASSARI.......................

Natoa pole nyingi kwa Shule ya Kikatiti Sec. kwa janga la kuungua bweni la wavulana.
Nimelazimika kuacha bunge kuja kuwaona.
Tunamshukuru sana Mungu, kwa Kuwa hakuna mwanafunzi aliyejuruhiwa wala kupoteza maisha.
Together we stand, together we go.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI ALIPOKUWA SAFARINI KUTOKEA DODOMA KUELEKEA ARUSHA

kat01Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha sehemu mbalimbali wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha kwa njia ya barabara leo Mei 6, 2016. PICHA NA IKULU
kat1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.

kat2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.
kat3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua karanga kutoka kwa mjasiriamali mara baada ya kuwahutubia mamia ya wakazi wa Babati mkoani Manyara waliojitokeza katika eneo la Stendi ya Mabasi ya Babati Mkoani Manyara
kat4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Magugu mkoani Manyara wakati akielekea  Mkoani Arusha.
kat5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Stendi ya Mabasi ya Singida wakati alipokuwa njiania kuelekea Arusha.

kat6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa  Endasak  mkoani Manyara wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha kwa njia ya barabara.


kat7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Dareda mkoani Manyara waliojitokeza kumsalimia wakati akitokea Dodoma kuelekea mkoani Arusha. PICHA NA IKULU

Thursday, 5 May 2016

Joh Makini Don't Bother ft AKA Official Music Video YouTubevia torch...

UTALII:Tanapa yalipa kodi ya Sh bilioni sita

Pascal Shelutete

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limesema kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 lilitumia zaidi ya Sh bilioni sita kama kodi na michango ya maendeleo kwa jamii.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Meneja Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete.
Alisema Tanapa inajitegemea kwa asilimia 100 kwa mujibu wa hesabu zake za mwaka 2013/2014 zilizokaguliwa na makusanyo yalikuwa ni Sh bilioni 150.9.
“Makusanyo hayo ya shilingi bilioni 150.9 ni kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato vya shirika letu la umma ambapo matumizi yalikuwa shilingi bilioni 145.9 huku tukiichangia Serikali Kuu jumla ya shilingi bilioni 6.7 kama kodi,” alisema Shelutete.
Akitoa mchanganuo huo wa kodi hiyo, alisema Tanapa ililipa Sh bilioni 1.5 kama kodi, ikatoa Sh bilioni 2.5 kama michango kwa Mfuko Mkuu wa Hazina pia ikatoa Sh bilioni 1.5 kama mchango wa tozo kwa ajili ya kuendeleza utalii huku Sh bilioni 1.1 zikielekezwa katika miradi ya maendeleo ya jamii inayozunguka hifadhi mbalimbali nchini.
Shelutete alitoa ufafanuzi huo baada ya mapema wiki hii vyombo kadhaa vya habari kuripoti kwamba katika mwaka wa fedha wa 2013/2014, Tanapa ilifanya matumizi makubwa ya fedha zaidi ya mapato yake.
Taarifa hizo ziliwanukuu wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji (PIC) wakisema kwamba katika mwaka huo, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilionyesha kwamba Tanapa ilitumia zaidi ya Sh bilioni 151.7, ilhali mapato yalikuwa ni Sh bilioni 149.9; kukiwa na matumizi ya ziada ya Sh bilioni 1.8.
Pia Shelutete alisema hadi sasa bajeti ya Tanapa si tegemezi.
“Kwa kuzingatia changamoto za uhifadhi, makisio ya gharama za uhifadhi zimeonekana kuwa kubwa kuliko mapato tarajiwa na nakisi iliyojitokeza imelengwa kusaidiwa na wafadhili mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.
“Shirika huandaa bajeti zake za kila mwaka kwa kuangalia hali halisi ya mapato na matumizi yanayoendana na mapato yake, ikiwa ni pamoja na kukasimia kodi mbalimbali na michango ya Serikali Kuu,” alisema Shelutete.
Alisema Tanapa ina Mpango Mkakati wa Shirika (CSP) wa mwaka 2013/2014 hadi mwaka 2017/2018 ulioandaliwa kwa ajili ya kuonyesha hali halisi na gharama stahiki za uendeshaji wa shughuli za uhifadhi kwa kipindi tarajiwa.
“Tafsiri ya mpango huu katika fedha huchukua taswira ya hali halisi ya changamoto za uhifadhi. Mpango mkakati huo umeandaliwa kwa minajili vile vile ya kuwaeleza wadau wa uhifadhi changamoto na upungufu wa gharama za uhifadhi. Nakisi inaonekana katika mpango mkakati inatarajiwa kufidiwa na wadau wa maendeleo na uhifadhi,” alisema Shelutete.

Agriculture:Arusha to host Banana production

Researchers from around the world are meeting

Researcher from around the world are meeting these week in Arusha to implement a five years project on improving banana production and productivity in Tanzania and Uganda.Their four-day meeting will take place at the Nelson Mandela Africa Institution of science and technology in Arusha
The event will involve Australian,Brazilian,Ugandan,Swedish,Belgium,South african and US expert.
The international institutes of tropical agriculture(IITA)project manager and soil specialist Mr. Danny Coyne said the project aimed strengthening banana breeding progammes ina Uganda and Tanzania to dramatically upscale andspeed up efforts in developing new high-yielding and diseases-resistant hybrid varieties

Tuesday, 3 May 2016

MAHAKAMA:Mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha...............

MKUU wa Chuo cha Uhasibu (IAA) Njiro mkoani Arusha, Profesa Johannes Monyo amehukumiwa kifungo cha nje kwa sharti la kutofanya kosa lolote ndani ya mwaka mmoja.
Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Msofe baada ya kujiridhisha kuwa Profesa Monyo alifanya makosa ya kuajiri watumishi wanane wenye elimu ya darasa la saba bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma.
Hakimu Msofe alisema Profesa Monyo akiwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro, aliwaingiza watumishi wanane kwenye ajira ya kudumu bila ya kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Mkuu Utumishi.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani kwa mashahidi 10 pamoja na vielelezo vinane vilivyotolewa mahakamani hapo na upande wa mshtakiwa kuwa na mashahidi wawili, mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kuwa Profesa Monyo alifanya kosa hilo la kuajiri wafanyakazi hao wanane bila kufuata taratibu za kisheria.
“Mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa ulifanya kosa hili la kuajiri wafanyakazi wanane bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma hivyo mahakama hii inakutia hatiani kwa kukupa kifungo cha nje kwa sharti la kuutofanya kosa lolote katika kipindi cha mwaka mmoja,” alisema Hakimu Msofe.
Awali, Mwanasheria kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Adam Kilongozi alidai kuwa Juni, 2010 Profesa Monyo anatuhumiwa kuwapa ajira watumishi wanane ambao ni Pamela Maboko, Samson Mbarya, Mawazo Ndaro, Juma Nyarutu, Lilian Ngowi, Godfrey Mollel, Musa Maiki na Salim Shabani.
Kosa jingine ni Profesa Monyo kwa kutumia mamlaka yake vibaya, kuwaingiza watumishi hao wanane katika ajira, ilhali akijua elimu zao ni darasa la saba. Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo kutolewa, Profesa Monyo ameonesha kusudio la kukata rufaa kupitia kwa wakili wake, Severine Lawena.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa, gazeti hili lilimhoji Mwanasheria wa Takukuru, Kilongozi, kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma au Kanuni zake inasemaje juu ya mtumishi anapohukumiwa akiwa bado yupo kazini, ambapo alisema kama mtuhumiwa amehukumiwa na akaonesha nia ya kukata rufaa, basi hukumu hiyo inaweza kufanya kazi au kutofanya kazi hadi hapo rufaa itakaposikilizwa.

Alisisitiza kuwa Takukuru wameshatuma nakala hiyo ya hukumu Tume ya Utumishi wa Umma, mwajiri wa Profesa Monyo, ili mamlaka husika zilifanyie kazi suala hilo lakini pia ni lazima mwajiri wake naye ajiridhishe na hukumu hiyo.

KILIMANJARO:Mkuu wa wilaya ya moshi awataka wajasiriamali kutengeneza bidhaa bora...............

MKUU wa Wilaya ya Moshi, Norvatus Makunga, amewataka wajasiriamali wadogo mkoani Kilimanjaro, kutengeneza bidhaa zenye ubora inayolingana na thamani halisi, kwa kupunguza uagizwaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Makunga aliyasema hayo jana mjini Moshi, wakati akifunga mafunzo ya wiki mbili ya wajasiriamali wadogo, wa fani mbalimbali kutoka wilaya za Moshi, Mwanga na Rombo, ambapo yaliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO).
Alisema tatizo kubwa la baadhi ya wajasiriamali wadogo hapa nchini, wamekuwa wakizalisha bidhaa nzuri lakini zimekuwa zikikosa ubora unaohitajika kwenye mahitaji ya soko, hali inayowafanya wafanyabiashara kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi.
Makunga alisema ubora wa bidhaa ndio nguzo muhimu ya kuweza kukuza soko la ndani na nje ya nchi, ambapo aliwataka wajasiriamali hao kujifunza na kujiimarisha zaidi, ili waweze kuwa washindani wazuri katika soko la Afrika masariki Mmoja wa wajasiriamali katika mafunzo hayo, Gloria Mosha, alisema changamoto inayowakabili wajasiriamali wadogo ni wafanyabiashara wakubwa kuagiza bidhaa nje ya nchi, ambapo bidhaa hizo zimekuwa zikitengenezwa hapa nchini, hali inayosababisha wajasiriamali kukosa soko la ndani.
Mosha alisema licha ya ubora wa baadhi ya bidhaa za ndani kutokidhi mahitaji ya soko la dunia, changamoto kubwa wanayokumbana nayo pia ni ukosefu wa nishati ya uhakika, hali inayosababisha ufanyaji kazi kuzorota kutokana na umeme kukatika mara kwa mara.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO), Arthur Ndedya, aliwataka washiriki hao kutumia mafunzo hayo, kwa lengo la kuboresha bidhaa zao zikidhi viwango vya ushindana wa masoko la dunia

SIASA:Sumaye ahimiza waandishi wa habari nchiikuzingatia maadili




WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kufanya kazi zao kwa utaratibu na kufuata miiko na maadili ya taaluma yao na kutakiwa kutojiingiza katika mambo ambayo ni kinyume na taaluma ya uandishi wa habari.
Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Siasa (TAPOREA) na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
“Tasnia ya habari ina utaratibu wake na miiko yake na ninyi lazima mtii miiko hiyo…msijiingize katika mambo ambayo ni kinyume kabisa cha taaluma yenu,” alisema Sumaye. Sumaye alisema uhuru wa habari una pande mbili, hivyo mmoja usizuiwe kutafuta, kupokea na kusambaza habari na upande wa pili ni mwandishi kufanya kazi kwa kufuata utaalamu na miiko ya taaluma yenyewe.
Alisema mwandishi ukiandika habari za uongo bila kuzithibitisha ni makosa, lakini pia ni makosa kuandika kwa kumuandama mtu au kikundi kwa kumchafua kwa makusudi. Alisema mwandishi ukimwandika mtu vibaya kwa sababu umelipwa fedha; au ukiacha kuandika ukweli kwa sababu hiyo hiyo ya kulipwa fedha au ya kutishiwa, nayo ni makosa.
Sumaye alisema kufanya hivyo, kunavifanya vyombo vya habari vidharauliwe na hata kushitakiwa na kutakiwa kulipa fidia kubwa kwa kuvunja heshima ya watu au mtu. “Siyo sifa gazeti lako kuonekana linaandika habari za uwongo kila mara au dhahiri linatumika na kikundi fulani ili kuchafua kikundi kingine, labda kwa mashindano ya kibiashara au kisisasa, kama ambavyo tunashuhudia wakati wa chaguzi mbalimbali,” alisema Sumaye.
Aidha, akizungumzia juu ya kuzuia matangazo ya Bunge kuoneshwa moja kwa moja, Sumaye alisema kufanya hivyo ni kuvunja Katiba Ibara ya 18 (d) kuwa kila mtu ana haki ya kupewa taarifa wakati wote na kuzuia matangazo hayo hakuendani na mfumo wa demokrasia.


Monday, 2 May 2016

MEI MOSI:Mkuu wa Mkoa wa Arusha ahutubia Wafanyakazi siku ya kilele cha mei mosi


S9Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa katika sherehe za mei day kabla ya kuwahutubia wafanyakazi Leo jijini Arusha katika uwanja wa sheikh Amri Abeid 
S6Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Ntibenda akihutubia wakazi na wafanyakazi wa mkoa wa Arusha wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi duniani Leo kwenye uwanja wa sheikh amri karume.
S10Wafanyakazi wa kampuni na mashirika mbalimbali mkoani Arusha wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha daud ntibenda hayupo picha kwenye kilele cha sherehe za wafanyakazi Leo jijini Arusha
S7Zawadi za washindi wa maonyesho ya mei mosi kama zinavyoonekana pichani .
S8Moja ya gari la maonyesho kwenye mei mosi la idara ya misitu kama lionekanavyo pichani.
S1Msafara wa magari ya maonyesho ukielekea uwanja wa sheikh amri Abeid jijini Arusha.
S2TAWIRI nao hawakuwa nyuma kwenye maonyesho ya mei mosi mkoani Arusha .

S4TBL nao pia wakikuwepo kwenye maonyesho hayo ya mei day
S3A to Z nao pia hawakuwa nyuma kwenyw siku ya mei mosi
S5Pichani ni magari ya maonyesho yakielekea uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.