Arusha
Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amelitaka shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na shirika la ushindani wa haki kuhakisha ifikapo July moja wanamaliza bidhaa zote bandia na zilizo chini ya viwango na wasipo fanya hivyo ajira zao zitafutwa mara na bidhaa hizo kuteketezwa.
Tamko hilo amelitoa waziri Charles Mwijage leo hii wakati alipokuwa anatembelea kujionea bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kusibitishwa ubora wake katika siku ya viwango afrika ambapo kwa upande wa kampuni ya cement ya Dangote afisa mkuu masoko Joel Laizer amemhakishi a waziri ubora wa cement zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Wakati huo huo kampuni ya Azania pamoja na Azam kwa kupitia kwa maofisa wao akiwemo Maofisa masoko afisa mkuu wa masoko wa AZANIA Naifa Abubakari pamoja Ibrahimu Masome wa AZAM wamemuhakikishia waziri wa viwanda biashara na uwekezaji kuwa wao wamejipanga vizuri kuhakisha wanatoa bidhaa zinazokidhi viwango bora na zenye ushindani na masoko kote duniani
Aidha kwa upande wao kampuni ya kuzalisha Bodi za magari ya kitalii pamoja na vyuma vya kujengea Maghala ya viwanda afisa biashara Mohan Krishan amemwambia waziri kuwa wao kama kampuni ya HANSPAUL wataakikisha wanatengeneza bidhaa bora zenye bei nafuu.
No comments:
Post a Comment