Sunday, 5 June 2016

ARUMERU:VYANZO VYA MAJI VINATAKIWA VILINDWE,SIKU YA MAADHIMISHO YA MAZINGIRA DUNIANI



Muu wa wilaya ya Arumeru,Wilson Nkambaku aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika shule ya Msingi Kiranyi.Ameagiza wananchi wote waliojenga kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya vyanzo vya maji wabomeo wenyewe.



Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya mji mdogo wa Ngaramtoni Sophia Shoko akizungumza jambo katika maadhimisho hayo



Diwani wa Kata ya Kiranya Halmashauri ya wilaya Arusha akiwataka wananchi kutii sheria hili kulinda vyanzo vya maji.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Wilson Nkambaku (katikati) aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha akifurahi jambo na katibu tawala (RAS)Richard Kwitega(kulia)kushoto katibu tawala Msaidizi huduma za afya,Hargeney Chitukulo.




Wanafunzi wa shule ya msingi ya serikali ya mchepuo wa Kiingereza ya Arusha school wakiimba shairi lao lenye kuhamasisha utunzaji wa Mazingira na kupanda miti.




Baadhi ya viongonzi kutoka Halmashauri ya Arusha DC wakimsikiliza kwa makini hotuba ya mkuu wa wilaya.



Baadhi ya viongonzi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha wadau wa taasisi binafsi na wananchi kwa pamoja wameshiriki kikamilifu  siku ya mazingira duniani..



Baadhi ya mabalozi wa taasisi ya vijana wa umoja wa mataifa (UN)walioshiriki maadhimisho hayo katika shule ya kiranyi.



Katibu tawala(RAS)mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akipanda mti katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani




Mrembo Morine Ayub Mollel ambaye ameshinda taji la Miss Arusha akipanda mti kwenye bustani ya shule msingi kiranyi.

No comments:

Post a Comment