Friday, 17 June 2016

UVCCM MKOA WA ARUSHA WALAANI VIKALI SHUTUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA


Na Mahmoud Ahmad Arusha
UMOJA wa vijana mkoa wa Arusha umelaani vikali kitendo cha jenerali Twaha ulimwengu kumkashifu Rais Mstaafu na mwenyekiti wa CCM taifa, Dkt Jakaya Kikwete kwa madai kuwa ashitakiwe mahakamani kwa kutumia fedha za umma vibaya kwa kuanzisha mchakato wa katiba ambao ulikwama kufikia tamati yake
 
Akitoa tamko hilio mbele ya wana habari mkoa wa Arusha mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha  Lengai Ole sabaya  alisema kuwa matamshi ya upotosha ji yaliyotolewa na jenerali twaha ulimwengu ni ya kupotosha umma
 
Aliongeza kuwa kutokana na matamshi hayo UVCCM wanamtaka jenerali aache kupotosha ukweli kama ulivyo kwani mchakato bado haujakwama ila umezingwa na miingiliano ya vipindi vya uitishaji wa kura ya maoni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
Aidha idhini ya matumizi ya fedha za mchakato wa Katiba ziliweza kuiidhinishwa na bunge kwa nia ya dhamira njema ya taifa ya kuandika katika yake mpya na wala sio ubadilifu au matumizi mabaya kama anavyotaka jenerali huyo.
 
Sabaya alisema kuwa alichokionesha jenerali mbele ya kadamnasi na vyombo vya habari ni kejeli pamoja na dharau isiyo staili kwani alionekana kujawa na nyongo kutokana na kumbukumbu zile za kuwekwa kando na utawala wa mkapa kasha kuzikwa kwenye kaburi la sahau utawala wa kikwete.
 
Aidha kutokana na matasmhi hayo umoja huo umewaomba na kuwasihi watanzania kuwa makini na kutuipilia mbali sanjari na kuweka tahadhari kwa watu wenye matamshi ya hamaki pamoja na hasira ambao wana nia mbaya ya kubomoa taifa.
 
Kutokana na hilo pia umoja huo umesema kuwa endapo kama ataendelea basi wao hawataweza kumtambua tena kama mwanachama mwenzao na pia watashinikiza hata uanachama wake utiliwe shaka kabisa

No comments:

Post a Comment