Wednesday, 29 June 2016

UBUNGE WA OLE NANGOLE LONGIDO WATENGULIWA NA MAHAKAMA KUU ARUSHA


images


Kesi iliyokuwa ikiunguruma kuanzia  Februari 29 ,2016 katika Mahakam Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii
Katika
shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt
Kiruswa  alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi
dhidi ya mbunge wa Longido Mh.Onesmo Nangole.
Akisoma hukumu
hiyo,Jaji Mwagesi  alisema kuwa mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa
na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.Katika shauri
hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo
Kutokana
na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa
pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka
mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;”Kutokana na kuzingatia
viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa
sheria,Natamka kwamba;
Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa
kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo
mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

Friday, 24 June 2016

MOSHI:WAZIRI MWIGULU AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA POLISI NA UHAMIAJI NAMBA 1/2015/2016, CCP MJINI MOSHI

g1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkabidhi zawadi mhitimu Irene Joji (kushoto) kwa kufanya vizuri katika masomo yake wakati wa mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba mjini humo leo.
g3Wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji wakimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) jinsi miili yao ilivyokuwa imara kwa pikipiki kupita juu ya matumbo yao. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba
g4Kikosi cha gwaride la heshima kikitoa heshima mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto jukwaa kuu) wakati wa sherehe yao ya kumaliza mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji, Chuo cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo
g5Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akisalimiana na Naibu Inspekta Jenerali  wa Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika viwanja vya Chuo Cha Polisi (CCP), mjini Moshi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji, kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

ANAJISIWA KISHA KUVUNJWA SHINGO


Mtoto wa miaka minne amejinasiwa kisha kuvunjwa shingo na kutupwa kando kando ya njia wanaopitaa wanaotembea kwa miguu karibu na mfereji wa maji mita 50 kutoka nyumbani kwao anapoishi Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamishina mkuu wa polisi wa jiji la Arusha Yusufu Ilembo, Tukio hili la kunajisiwa kwa mtoto limetokea Juni 20, mwaka huu saa 03:30 usiku kwenye makaburi ya Baniani kata ya unga limited.
Kaimu kamishina wa Polisi wa Jijini hapa Arusha jan alisema mtoto huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa akicheza na wenzake  nje kidogo ya nyumba yao na ilipofika saa 12:00 jioni kwa majibu ya marafiki zake (majina yamehifadhiwa) alifika mtu mmoja mwanaume mrefu,Kwa mujibu ya watoto hao mwanaume alikuwa amevaa suruali na kumwambia mtoto huyo amfate akamnunulie pipi  na hapo ndipo alipomfuata mwanaume huyo na akurudi tena mpaka alipokutwa ameshauwawa kikatilii.

Wednesday, 22 June 2016

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA SIKU YA VIWANGO BARANI AFRIKA


index


Arusha
Waziri wa Viwanda  Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amelitaka shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na shirika la ushindani wa haki kuhakisha ifikapo July moja  wanamaliza bidhaa zote bandia na  zilizo chini ya  viwango na wasipo fanya hivyo ajira zao zitafutwa mara na bidhaa hizo kuteketezwa.
Tamko hilo amelitoa waziri Charles Mwijage leo hii wakati alipokuwa anatembelea kujionea bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kusibitishwa ubora wake katika siku ya viwango afrika ambapo kwa upande wa kampuni ya cement ya Dangote afisa mkuu masoko Joel Laizer amemhakishi a waziri ubora wa cement zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Wakati huo huo kampuni ya Azania pamoja na Azam kwa kupitia kwa maofisa wao akiwemo Maofisa masoko  afisa mkuu wa masoko wa AZANIA  Naifa Abubakari pamoja Ibrahimu Masome wa AZAM  wamemuhakikishia waziri wa viwanda biashara na uwekezaji kuwa wao wamejipanga vizuri kuhakisha wanatoa bidhaa zinazokidhi viwango  bora na zenye ushindani na masoko kote duniani
Aidha kwa upande wao kampuni ya kuzalisha Bodi za magari ya kitalii pamoja na vyuma vya kujengea Maghala ya viwanda afisa biashara Mohan Krishan amemwambia waziri kuwa wao kama kampuni ya HANSPAUL  wataakikisha wanatengeneza bidhaa bora zenye bei nafuu.

SAGCOT WASAINI MKATABA NA MAKAMPUNI YALIYOOMBA UFADHILI KWA AJILI YA UKUZAJI KILIMO NA VIWANDA

01Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na vongozi wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.
1Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo (Mwenye tai nyekundu waliosimama) akishuhudia  wawakilishi wa vyama vya wakulima wakisaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko huo jijini Dar es Salaam leo. wanaosaini hati hizo kutoka kulia ni Mkulima wa miwa Dk George Mlingwa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Germao Cane Estate, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe, Roy Omulo kutoka kiwanda cha Maziwa cha Asas Dairies Iringa  na Lutengano Peter Mwenyekiti wa MUWAMARU Tukuyu mkoani Mbeya.
02Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo amesema kuwa Mfuko wa SAGCOT wamesaini mikataba kwaajili ya kibiashara kwanzia mtaji kati ya Dola Za Kimarekani milioni 50 hadi 100 zitakuwa zikitolewa  kwa miradi kupitia madirisha ya Matching Grant Fund(MGF) ambao utakuwa ukitatua changamoto za wakulima na masoko yao.
2
Baadhi ya viongozi hao wakiwa katika mkutano huo leo
3
Baadhi ya wafadhili wakiwa katika mkutano huo
4
Washiriki wa mkutano huo kutoka makampuni mbalimbali na serikali
5Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe wakati wa mkutano huo

Friday, 17 June 2016

UVCCM MKOA WA ARUSHA WALAANI VIKALI SHUTUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA


Na Mahmoud Ahmad Arusha
UMOJA wa vijana mkoa wa Arusha umelaani vikali kitendo cha jenerali Twaha ulimwengu kumkashifu Rais Mstaafu na mwenyekiti wa CCM taifa, Dkt Jakaya Kikwete kwa madai kuwa ashitakiwe mahakamani kwa kutumia fedha za umma vibaya kwa kuanzisha mchakato wa katiba ambao ulikwama kufikia tamati yake
 
Akitoa tamko hilio mbele ya wana habari mkoa wa Arusha mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha  Lengai Ole sabaya  alisema kuwa matamshi ya upotosha ji yaliyotolewa na jenerali twaha ulimwengu ni ya kupotosha umma
 
Aliongeza kuwa kutokana na matamshi hayo UVCCM wanamtaka jenerali aache kupotosha ukweli kama ulivyo kwani mchakato bado haujakwama ila umezingwa na miingiliano ya vipindi vya uitishaji wa kura ya maoni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
Aidha idhini ya matumizi ya fedha za mchakato wa Katiba ziliweza kuiidhinishwa na bunge kwa nia ya dhamira njema ya taifa ya kuandika katika yake mpya na wala sio ubadilifu au matumizi mabaya kama anavyotaka jenerali huyo.
 
Sabaya alisema kuwa alichokionesha jenerali mbele ya kadamnasi na vyombo vya habari ni kejeli pamoja na dharau isiyo staili kwani alionekana kujawa na nyongo kutokana na kumbukumbu zile za kuwekwa kando na utawala wa mkapa kasha kuzikwa kwenye kaburi la sahau utawala wa kikwete.
 
Aidha kutokana na matasmhi hayo umoja huo umewaomba na kuwasihi watanzania kuwa makini na kutuipilia mbali sanjari na kuweka tahadhari kwa watu wenye matamshi ya hamaki pamoja na hasira ambao wana nia mbaya ya kubomoa taifa.
 
Kutokana na hilo pia umoja huo umesema kuwa endapo kama ataendelea basi wao hawataweza kumtambua tena kama mwanachama mwenzao na pia watashinikiza hata uanachama wake utiliwe shaka kabisa

Wednesday, 8 June 2016

MKUU WA MKOA WA ARUSHA ATEMBELEA SAFARI CITY KUJIONEA MAENDELEO YA KAZI KABLA YA UZINDUZI

 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Daudi Ntibenda akiwasili katika eneo la Safari City kuona maendeleo ya mradi huo na kulakiwa na Meneja wa NHC Mkoa wa Arusha, James Kisarika. Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Kamati yake nzima ya Ulinzi na Usalama, wametembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.
Mmoja wa viongozi wa kamati yake nzima ya Ulinzi na Usalama ya Arusha akisalimiana na Afisa Mauzo wa NHC, Mariam Chisumo wakati kamati hiyo ilipotembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.
Meneja wa NHC mkoa wa Arusha,  James Kisarika akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Daudi Ntibenda ramani ya eneo la Safari City wakati kamati yake nzima ya Ulinzi na Usalama ya Arusha  ilipotembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.
 Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Daudi Ntibenda ukiwasili eneo la Tukio.
 Meneja wa NHC mkoa wa Arusha, James Kisarika akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Daudi Ntibenda ramani ya eneo la Safari City wakati kamati yake nzima ya Ulinzi na Usalama ya Arusha  ilipotembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.
Kamati yake nzima ya Ulinzi na Usalama, wakiangalia maendeleo ya Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo.
 Meneja wa NHC mkoa wa Arusha, James Kisarika akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Daudi Ntibenda ramani ya eneo la Safari City wakati kamati yake nzima ya Ulinzi na Usalama ya Arusha  ilipotembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.
 Meneja wa NHC mkoa wa Arusha, James Kisarika akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Daudi Ntibenda ramani ya eneo la Safari City wakati kamati yake nzima ya Ulinzi na Usalama ya Arusha  ilipotembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.
 Upimaji ukiendelea
 Uchongaji wa barabara ukiendelea.
 Upimaji ukiendelea.
 Uchongaji barabara ukiendelea.
 Jiwe linaloonyesha mojawapo ya mipaka.
 Meneja wa NHC mkoa wa Arusha akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Daudi Ntibenda ramani ya eneo la Safari City wakati kamati yake nzima ya Ulinzi na Usalama ya Arusha  ilipotembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.
 Meneja wa NHC mkoa wa Arusha, James Kisarika akimkaribisha Diwani wa Mererani, Justin Nyari na wa Mateves, Robert Katara  ilipotembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.
 Meneja wa NHC mkoa wa Arusha, James Kisarika akimkaribisha Diwani wa Mererani, Justin Nyari na wa Mateves, Robert Katara  ilipotembelea Safari City kuona maendeleo ya utengenezaji barabara za Safari City na ugawanyaji wa maeneo tayari kwa uzinduzi wa uuzaji wa viwanja Jumamosi tarehe 11/6/2016.