Saturday, 30 April 2016

MKUU WA MKOA ARUSHA:Amepiga maarufuku unywaji wa viroba.........

Mkuu wa mkoa wa Arusha yetu Ndugu Felix Ntibenda amepiga maarufuku unywaji  na vinywaji cha kilevi aina ya kiroba kwa wakazi wa Arusha,Alisema uamuzi ameuchukua umetokana na vijana wa arusha ambao ni nguvu kaziya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.
Aidha mkuu wa mkoa wetu anafanyia kazi sakata la mkazi wa kata ya ngarenaro anayedaiwa kujihusiaha na biashara ya uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha.
Ntibenda aliyazungumza jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa 154,maofisa watendaji kata 25, pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa.
Alisema pia kutokana na vijana kunywa kinywaji  hicho nyakati za kazi amepiga maarufuku uuzaji wa kinywaji hicho.......alisema suala la kilevi cha kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki,daladala na wapiga debe.
"sitaki kuona viroba vikiuzwa katika mkoa wa arusha  na atakeyekiuka nitamchukulia hatua za kisheria,lakini huyu anayeuza madawa ya kulevya  halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajua kwanini anahachiwa huku akiendelea kuuza dawa hizi sasa namwambia mwisho wake umefika"

No comments:

Post a Comment