Saturday, 30 April 2016

HALI YA HEWA ARUSHA:Leo na kesho manyunyu na radi............

 Leo Jumapili tarehe 30 april Manyunyu au mvua ya radi joto ni nyunzi 27 chini 17
Kesho Jumapili tarehe 1 may manyunyu au mvua ya radi joto nyunzi 27 chini 17
Jamatatu tarehe 2 May Mawingu mengi na mvua ya radi joto nyunzi 28 chini16
Jumanne tarehe 3 May Mawingu mengi joto nyunzi 26 chini 16
Jamatano tarehe 5 May mawingu joto nyunzi 27 chini 17
 Ramani ikionyesha taswira na uota wa asili wa mkoa wa Arusha
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya utabibiri wa hali ya hewa(TMA)Bi. Kijazi akiongea na waandishi wa habari

MKUU WA MKOA ARUSHA:Amepiga maarufuku unywaji wa viroba.........

Mkuu wa mkoa wa Arusha yetu Ndugu Felix Ntibenda amepiga maarufuku unywaji  na vinywaji cha kilevi aina ya kiroba kwa wakazi wa Arusha,Alisema uamuzi ameuchukua umetokana na vijana wa arusha ambao ni nguvu kaziya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.
Aidha mkuu wa mkoa wetu anafanyia kazi sakata la mkazi wa kata ya ngarenaro anayedaiwa kujihusiaha na biashara ya uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha.
Ntibenda aliyazungumza jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa 154,maofisa watendaji kata 25, pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa.
Alisema pia kutokana na vijana kunywa kinywaji  hicho nyakati za kazi amepiga maarufuku uuzaji wa kinywaji hicho.......alisema suala la kilevi cha kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki,daladala na wapiga debe.
"sitaki kuona viroba vikiuzwa katika mkoa wa arusha  na atakeyekiuka nitamchukulia hatua za kisheria,lakini huyu anayeuza madawa ya kulevya  halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajua kwanini anahachiwa huku akiendelea kuuza dawa hizi sasa namwambia mwisho wake umefika"

MASHIRIKA:Mwanzilishi wa Taasisi ya Man at work akutana na wadau wake Jijini Arusha

 Mwanzilishi wa taasisi ya wanaume man at work Maxwell Stansalaus akizungumza na wanaume wa jijini arusha katika mkutano mkuu wa wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na wanaume 700 ambao lengo lilikuwa kuhamasisha wanaume na wajibu wao katika jamii.

Taasisi isiyo ya  kiserikali ya Wanaume Kazini maarufu kama Man at Work imelaani vikali vitendo vya ushoga vinavyoshusha hadhi na thamani ya wanaume hivyo wameitaka serikali kupiga vite vitendo hivyo ambavyo ni kunyume cha Maadili ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla.
Muasisi wa Taasisi hiyo  yenye makao yake jijini Arusha Maxwell  Stanslaus  amesema kuwa Wanaume kazini wanapinga vikali vitendo vya ushoga kwa zaidi ya Asilimia 100% na kuwataka wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha Mara moja.
Maxwell alisema hayo jana katika mkutano Mkuu wa Wanaume kazini uliofanyika jijini hapa huku akisema kuwa taasisi hiyo imelenga kuhimiza wanaume kote nchini kutimiza wajibu wao na kutenda majukumu yao kama wanaume katinga ngazi ya familia,jamii na taifa ili kuchochea maendeleo.
“Kwa sasa tunaona nidhamu ya serikali imerudi kutokana na Mwanaume mmoja tu Rais John Pombe Magufuli kuamua kutimiza wajibu yake hivyo Basi  Wanaume zaidi ya Milioni  walioko Tanzania wakiamua kutimiza majukumu yao na wajibu Tanzania itanyooka” Alisema Maxwell
Moja kati ya Wanaume waliohudhuria ni Joseph Mayagila alisema kuwa matatizo ya ushoga yanatokana na baadhi ya wanaume kujisahau na kujaribu kuwa wanawake ,jukwaa hili la wanaume ni muhimu kuwakumbusha wanaume juu ya uanaume wao na kutimiza yale yanayowapasa kama wanaume.
Dokta Emmanuel Buganga  ameeleza kuwa vuguvugu la wanawake kudai haki zao linatokana na baadhi ya wanaume kutotimiza wajibu wao kama wanaume wameacha majukumu yao ya kutunza familia zao na kuwa walezi na walinzi wa familia . 
Mhamasishaji wa Masuala ya kijamii Samuel Sasali amesema kuwa wanaume wengi wamejisahau sana katika masuala ya malezi ya familia kwani usimpolea mtoto katika njia impasayo atakuja kukuaibisha ukubwani.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na taifa.by Arusha yetu repoter

BUNGENI:Mbunge wetu wa Arusha mjini amechangia hoja katika wizara ya ofisi ya raisi,Tamisemi,utumishishi na utawala bora

Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema(CHADEMA) akichangia hoja wakati wa kujadili hoja ya hotuba ya Bajeti ys ofisi ya rais,Tamisemi,utumishi na utawala bora jana bungeni.

Dogo Janja My Life Official Music Video/Arusha yetu

G Nako OG Original Official Video/arushayetu

Friday, 29 April 2016

Karibu Arusha....................kwa utalii,mandhari,ukarimu,burudani na zaidi

 Njoo uone na upande mnyama aina ya ngamia
 Njoo ujionee utamaduni uliobaki Afrika
 Njoo upande usafiri wa ngamia
 njoo ujione wanyama wa aina mbalimbali

 Njoo uone siasa iliyokomaa
 Njoo uone viongozi makini na jasiri mithili ya simba
 Njoo uonee hifadhi za kuvutia
Njoo umuone mbunge na kiongozi kijana mdogo......aaaaah aaaaah Arusha ndio yetu

Pata taarifa zote za Arusha sasa..........

Pata matukio yote ya Jijini Kwetu arusha kwa kuvisit blog hii,follow twitter arusha_yetu,facebook arusha yetu