Monday, 15 August 2016

WAZIRI NAPE AFUNGA MASHINDANO YA GOFU YA WAZI YA TANZANIA JIJINI ARUSHA,WAKENYA WATAMBA

1
Richard Owiti kutoka nchini Kenya akionesha kombe lake la ushindi mara baada kushika nafasi ya kwanza kwa wachezaji wa ridhaa,kwenye mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye (wa pili kulia).Kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango wakishuhudia kwa pamoja.


Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi vifaa vya mchezo huo wa Gofu mshindi wa kwanza wa wachezaji wa ridhaa katika Mashindano ya Gofu ya wazi ya Tanzania,Richard Owit kutoka nchini Kenya,yaliofungwa jana jioni katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha,pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango. Mashindano hayo yaliyokuwa na msisimko mkubwa yalishirikisha washiriki wapatao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Kenya na Unganda. 
Mshindi wa kwanza kwa wachezaji wa kulipwa wa mchezo huo wa Gofu kutoka nchini Kenya,Jacob Okelo akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni sita,kwenye hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania ,yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya USA River na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja Afisa Maendeleo ya jamii na Uhusiano,Justine Kesi ikiwa ni sehemu ya kiasi cha fedha kilichotolewa na Wadhamini waliodhamnini mashindano hayo ya Gofu kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya huduma za jamii mbalimbali kwa vijiji vinavyozunguka viwanja vya Kili Golf,jijini Arusha.

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali jana jioni wakati wa kufunga mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf- USA River  jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo wageni waalikwa wakiwemo wachezaji wa kulipwa na ridhaa wa mchezo huo walishiriki.PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhidia hitmisho la mashindano hayo ya gofu,wakifuatilia hotuba fupi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Nape

Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhidia hitmisho la mashindano hayo ya gofu,wakifuatilia hotuba fupi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Nape

Wazir Nape (wanne kulia) akiwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wa Gofu hapo jana kabla ya kuhitimisha 
mashindano hayo

Baadhi ya Wadau nao walikuwepo kufuatilia kuhitimishwa kwa mashindano hayo ya Gofu jana jioni jijini Arusha

Waziri Nape pia alikutana na wadau ambao walidhamini mashindano hayo ya Gofu

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimsikiliza Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA),Mh Godbless Lema,kwenye viwanja vya Kiligolf,USA-River jijini Arusha,ambapo Mh Nape alikuwa mgeni rasmi katika kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania.Pichani kulia ni Diwani wa kata ya Maroroni,Mh.Bryason Issangya (CHADEMA)
Waziri Nape (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Gofu kwenye viwanja vya Kiligolf jijini Arusha,kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania,Chris Martin,Mkurugenzi wa viwanja vya Gofu (KiliGolf),Jerome Bruins,Mmoja wa wasimamizi waku wa kampuni ya Group Six International LTD,Janson Huang,na kushoto kwa Waziri ni Mke wa Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh Joshua Nassari,Mh Joshua Nassari,Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango pamoja na Diwani wa kata ya Maroroni,Mh.Bryason Issangya (CHADEMA)
Waziri Nape akishiriki kucheza mchezo wa Gofu

Waziri Nape akipata maelezo mafupi kuhusiana na uwanja huo wenye viwango vyote kimataifa cha Kiligolf.
Waziri Nape akifurahia jambo na Mhe Nassri,kulia ni Mke wa Mh Nassari

Waziri Nape pia alipata wasaa wa kutembelea mashimo ya mchezo huo wa Gofu yapatayo 18 ndani ya uwanja wa Kili Gofu,uliopo USA River jijini Arusha.

Monday, 1 August 2016

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS TAMISEMI AZINDUA KISIMA KILICHOCHIMBWA NA TAASISI YA KIDINI JIJINI ARUSHA


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo akizungumza kwenye mkutano wahadhara
kwenye soko maarufu la Kwamrombo kabla ya kuzindua kisima cha maji kwaajili ya matumizi ya wafanyabiashara wa soko hilo kilichochimbwa na taasisi ya kidini ya Ansaar MuslimYouth Centre tawi la Arusha .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo akizindua kisima cha maji kwenye soko maarufu la Kwamrombo kwaajli ya matumizi ya wafanyabiashara wa soko hilo kilichochimbwa na
taasisi ya kidini ya Ansaar MuslimYouth Centre tawi la Arusha .

Wananchi wakifurahia hotuba ya Naibu Waziri Jaffo ambaye alitumia mkutano huo kumwagiza Meneja wa Tanesco kuwaunganishia umeme mapema inavyowezekana.
Wananchi wakifurahia hotuba ya Naibu Waziri Jaffo ambaye alitumia mkutano huo kumwagiza Meneja wa Tanesco kuwaunganishia umeme mapema inavyowezekana.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro(kushoto) akimweleza jambo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo eneo la Olmoti kilipo kisima cha maji kinachowahudumia wananchi wa Kata ya Olmoti na Olasiti pia maji hayo yatatumika kwenye mahakama ya kimataifa ya MICT,kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Ruth Koya,Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo(katikati).

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo akipata maelezo kando ya Tenki la
kuhifadhia maji lenye ukubwa wa ujazo wa lita 60,000 lililopo Kata ya
Olmoti jijini Arusha.
 
Mkazi wa Kata ya Osunyai jijini Arusha akirekodi hotuba ya  Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo kwa kutumia simu yake.
Wananchi
wakifurahia hotuba ya Naibu Waziri Jaffo ambaye alitumia mkutano huo
kumwagiza Meneja wa Tanesco kuwaunganishia umeme mapema inavyowezekana.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia(katikati)akifafanua jambo

KAMPUNI YA OFF GRID YAJIBADILI JINA LA BIASHARA NA KUFUNGUA MADUKA MAPYA TANZANIA NA RWANDA

Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya Zola, akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo, jijini Arusha. 
Shughuli za uzinduzi wa duka hilo, jipya la vifaa vya umeme wa jua la Kampuni ya Zola, zikiendelea jijini Arusha. 
Wafanyakazi wa Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya Zola wakishangilia mara baada ya kukatwa utepe wa kulizindua rasmi duka hilo, jipya jijini Arusha.